Kamati ya michezo ya kampuni ya Softnet Technologies, leo imekabidhi vifaa vya michezo kwa shule ya msingi Mikocheni. Vifaa hivi ni pamoja na mipira na jezi kwa ajili ya mpira wa miguu. Msemaji wa kamati bwana Israel Nhayo amesema,

"Tunaamini kwamba michezo ni sehemu ya muhimu sana katika ukuaji wa mtoto, na pia kwa kuanza mapema wakiwa wadogo tunatengeneza vipaji ambavyo vitakuja kuwa na umuhimu mkubwa sana kwa Taifa letu, kwa hiyo kwa msaada huu mdogo wa jezi na mipira tunapenda kuunga mkono juhudi zinazofanywa na shule kwa ajili ya watoto hawa"

Bwana Nhayo pia alisistiza kuwa Softnet kama kampuni itaendelea kushirikiana na shule kuhakikisha watoto wanapata elimu iliyo bora kwa njanja zote.

Mwakilishi wa wanafunzi alipata nafasi ya kutoa shukrani zao kwa niaba ya wanfunzi wenzake, pia alipata nafasi ya kutoa ombi la misaada Zaidi kwa ajili ya vifaa Zaidi vya michezo kama magoli madogo ya mpira na magoli ya netball. Mwalimu wa michezo wa shule ya Mikocheni paia alipata nafasi ya kutoa shukrani zake kwa uongozi wa Softnet, na pia kuomba moyo wao wa upendo uendelee kwa manufaa ya watoto wa shule hiyo.