Zaidi ya taasisi 120 za elimu ya juu na utaafiti zinafungwa vifaa vya mtandao vitaavyoviunganisha na Mkonga wa Taifa ili kuziwezesha kupata rejea za masomo wanayochukua, mawasiliano na kuingia kwenye mfumo wa taarifa za kitaaluma za ndani na nje ya nchi.

Awamu ya kwanza vyuo vya elimu ya juu vitakavyounganishwa ni kutoka Mikoa ya Dar es salaam,Iringa,Arusha,Mbeya,Kilimanjaro,Morogoro na Zanzibar, likiwemo baraza la mitihani Tanzania (NECTA)

Elimu ya juu inategemea kupata manufaa toka maktaba , mradi huu utawawezesha wanafunzi kupata vitabu na taarifa kutoka chuo chochote duniani.Lakini natoa wito kwa wanafunzi na wanaoongoza taasisi za elimu nchini kuvithamini na kuvitunza na kuvitumia kwa manufaa mengine.