Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Mheshimiwa January Makamba (kulia) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SoftNet Technologies Limited, Nuru Yakub Othman, alipofanya ziara kukakugua hatua za utekelezaji wa mradi wa kuunganisha taasisi za Elimu ya Juu na za Utafiti zijulikanazo kama HERIs (Higher Education and Research Institutions).

Mradi huu unatekelezwa na kampuni ya SoftNet Technologies Limited (mkandarasi) na unalenga kuboresha miundo mbinu ya Tehama katika taasisi zaidi ya 120 ambapo awamu ya kwanza inahusisha takriban taasisi 28 zilizoko Dar Es Salaam, Morogoro, Zanzibar, Iringa, Mbeya, Dodoma, Arusha na Kilimanjaro. Mradi huu unafadhiliwa na Benki Ya Dunia kupitia Wizara Ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.